Mabehewa 264 ya mizigo ya reli ya SGR yaliyotengenezwa China yawasili Tanzania

(CRI Online) Desemba 26, 2024

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limepokea mabehewa 264 ya mizigo yaliyotengenezwa na kampuni ya CRRC Qiqihar ya China kwa ajili ya treni za umeme za reli ya SGR.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo, mabehewa 200 kati yao yatatumika kusafirisha makontena, na mengine 64 kwa mizigo ya kawaida.

Operesheni za kibiashara za mabehewa hayo zitaanza kufuatia TRC na wataalamu kutoka kwa wakandarasi kuidhinisha matumizi ya mabehewa hayo, baada ya usafiri wa majaribio kufanyika. Lakini halijasema majaribio yatafanyika lini.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha