

Lugha Nyingine
Sensa ya tano ya uchumi wa China yaonesha uhai mpya wa maendeleo
China imechapisha matokeo ya sensa ya tano ya uchumi wa taifa, ambayo inaonyesha kuwa katika miaka mitano iliyopita uchumi wa nchi umeendelea kuwa na msingi thabiti, ustahimilivu imara na uwezo mkubwa.
Pato la taifa la China (GDP) kwa mwaka 2023 lilifikia yuan trilioni 130 (takriban dola trilioni 18.08 za Marekani), na kuwa uchumi wa pili kwa ukubwa duniani. Wastani wa mchango wa nchi katika ukuaji wa uchumi duniani umeendelea kuwa karibu asilimia 30 kwa miaka mitano iliyopita, na kuifanya China kuwa injini kubwa zaidi ya ukuaji wa uchumi wa dunia.
Matokeo ya sensa pia yanaonesha kuwa muundo wa uchumi wa China uliendelea kuimarika. Sekta ya huduma iliendelea kuwa na umuhimu, na thamani yake iliyoongezwa ilichangia asilimia 56.3 ya Pato la Taifa kwa mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 2 kuliko mwaka wa 2018. Mkuu wa Idara ya Taifa ya Takwimu ya China Bw. Kang Yi pia amesema, China imeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya mashirika na watu walioajiriwa na sekta za uchakataji na huduma.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma