Zambia, Saudi Arabia zasaini makubaliano ya kurekebisha deni

(CRI Online) Desemba 27, 2024

Zambia na Saudi Arabia zimesaini makubaliano ya kurekebisha deni ili kupanga upya sehemu ya deni la Zambia inalodaiwa na Saudi Arabia.

Makubaliano hayo yalisainiwa na waziri wa fedha na mipango wa Zambia Bw. Situmbeko Musokotwane na ofisa mtendaji mkuu wa mfuko wa maendeleo wa Saudi Arabia Sultan Abdulrahman Al-Marsha huko Lusaka.

Chini ya makubaliano hayo, nchi hizo mbili zitapanga upya zaidi ya dola milioni 130 za deni la Zambia kwa Saudi Arabia. Nchi hizo mbili pia zimesaini makubaliano mengine ya kuidhinisha mkopo wa dola milioni 35 ili kufadhili ujenzi wa Hospitali Maalumu ya King Salman nchini Zambia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha