Umoja wa Afrika waeleza wasiwasi juu ya vurugu baada ya uchaguzi nchini Msumbiji

(CRI Online) Desemba 27, 2024

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat ameeleza wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa vurugu baada ya uchaguzi mkuu nchini Msumbiji, haswa kufuatia matokeo ya mwisho kutangazwa hivi karibuni na baraza la katiba la nchi hiyo, ambazo zimesababisha vifo vya watu.

Bw. Faki ametoa rambirambi kwa familia za wahanga, na kutaka kuwepo kwa utulivu na kuhimiza mamlaka za usalama za nchi hiyo kujizuia na kufuata sheria na utaratibu. Pia ametoa wito kwa serikali ya Msumbiji na pande husika za kisiasa na kijamii kujitahidi kutafuta suluhisho la amani kukabiliana na mgogoro wa sasa ili kuepuka vifo na uharibifu wa mali zaidi.

Pia amesisitiza tena ahadi ya Umoja wa Afrika ya kushirikiana na wadau husika wa Msumbiji na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika ili kukomesha vurugu na kulinda demokrasia ya kikatiba nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha