Sekta ya viwanda nchini Ethiopia yaboreka kwa uwezo wa uzalishaji, utoaji fursa za ajira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 27, 2024

ADDIS ABABA - Serikali ya Ethiopia imesema kuwa juhudi za hivi karibuni za kukabiliana na changamoto zinazokabili sekta ya viwanda nchini humo zimeongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wake wa uzalishaji na kutoa fursa za ajira.

Habari iliyotolewa jana na Shirika la Habari la Serikali ya Ethiopia zinasema kuwa, Waziri wa Viwanda wa Ethiopia Melaku Alebel amesema juhudi na mipango mbalimbali imetoa mchango katika ongezeko kubwa la uwezo wa uzalishaji wa sekta ya viwanda, ambao umeimarika kutoka asilimia 46 hadi asilimia takriban 60 ya jumla ya nchi hiyo katika miaka ya hivi karibuni.

Waziri huyo pia amesisitiza kuwa juhudi hizo zimeboresha kwa kiasi kikubwa uwezo wa jumla wa sekta hiyo wa uzalishaji ajira kwa mwaka, ambapo sekta ya viwanda sasa inatoa nafasi za ajira zaidi ya 156,000, ikiongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Huku soko la ndani la Ethiopia kihistoria likitegemea sana bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, Alebel amesema kuwa maboresho katika sekta ya viwanda yameongeza kiasi cha bidhaa zinazotengenezwa nchini humo pia, ambayo imepanda kutoka asilimia 30 hadi 40 katika miaka michache iliyopita.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka Shirika la Maendeleo ya Maeneo Maalum ya Viwanda la Ethiopia, uwekezaji wa China umetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya viwanda nchini Ethiopia, kwani wawekezaji wa China kwa sasa wanawakilisha kundi kubwa zaidi la wawekezaji wa kigeni katika maeneo ya viwanda nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa mwezi Oktoba, Kamisheni ya Uwekezaji ya Ethiopia ilisisitiza mchango muhimu wa wawekezaji wa China katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi ya Ethiopia, wakiingiza mtaji mkubwa, na kutoa fursa za ajira.

Ilisema miradi ipatayo 3,309 ya China imewekeza dola za Kimarekani zaidi ya bilioni 8.5 nchini Ethiopia katika miaka iliyopita, ikitoa mchango mkubwa katika kutimiza malengo ya nchi hiyo ya kijamii na kiuchumi. Uwekezaji huo pia umezalisha fursa za ajira za kudumu na za muda mfupi zaidi ya 325,400 kwa Waethiopia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha