

Lugha Nyingine
Kuelekea siku za baadaye bega kwa bega
"Dunia inakwenda wapi na binadamu wanapaswa kufanya nini?" Kwa kukabiliwa na kujibu swali hili la zama tulizonazo , Mwaka 2013, Rais Xi Jinping alitoa kwanza wazo la jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Mwezi Septemba mwaka huo, Rais Xi Jinping alitoa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ili kuunda jukwaa la kufanya uzoefu kwa ajili ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Katika muongo huo mmoja uliopita, ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja umeendelea kukua kutoka wazo la pendekezo hadi mfumo wa kisayansi, kutoka pendekezo la China hadi maoni ya pamoja ya kimataifa, kutoka matarajio mazuri hadi matokeo ya uzoefu, na usanifu wa ramani ya dunia nzuri ya binadamu unaelekea kuwa hali halisi hatua kwa hatua.
Mkondo wa zama za amani, maendeleo, ushirikiano na manufaa kwa pande zote hauzuiliki. Nchi zote duniani ziko kwenye meli moja yenye mustakabali wa pamoja. Tukiwa tunakabiliwa na mawimbi ya dhoruba, ni kwa kushirikiana pamoja tu ndipo tunaweza kusonga mbele kuelekea siku nzuri za baadaye.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma