Viongozi wa China watazama maonesho ya michezo ya Opera za jadi kwenye Tamasha la Usiku la Mwaka Mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 31, 2024

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, viongozi wengine wa Chama na serikali Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng wametazama maonesho ya michezo ya opera za jadi kwenye tamasha la usiku la Mwaka Mpya wa 2025 jana Jumatatu jioni mjini Beijing.

Viongozi hao wa China walitazama maonyesho hayo kwenye Jumba Kuu la Kitaifa la Maonesho ya Michezo ya Sanaa, pamoja na watu wa sekta mbalimbali mjini Beijing.

Kabla ya maonyesho kuanza, Rais Xi na viongozi wengine walishikana mikono na kusalimia wajumbe wa wasanii wa opera za jadi waliokuwa kwenye hadhira.

Kwenye tamasha hilo la usiku, michezo ya sanaa maarufu ya sehemu za opera za jadi imeonyesha ushujaa na upendo kwa China, vilevile imeonesha moyo wa watu wa zama tulizonazo na utamaduni wa taifa unaojaa nguvu ya uhai.

Michezo hiyo ya sanaa ilichaguliwa kutoka opera za jadi za aina mbalimbali, zikiwemo Opera ya Beijing na Opera ya Kunqu, zote mbili zimeorodheshwa kuwa mali ya urithi wa utamaduni usioshikika na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha