Madaktari wa China watoa huduma kwa wagonjwa wa Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 31, 2024
Madaktari wa China watoa huduma kwa wagonjwa wa Botswana
Hu Minxiong (kulia) akiwa katika picha pamoja na mwanafunzi wake Gomolemo Montsho katika Hospitali ya Rufaa ya Nyangabgwe mjini Francistown, mji wa pili kwa ukubwa nchini Botswana, Oktoba 24, 2024. (Picha na Shingirai Madondo/Xinhua)

GABORONE - Kelesetse Bosha kutoka kijiji cha Semotswane, kilichoko umbali wa kilomita 30 kusini-magharibi mwa Francistown, mji wa pili kwa ukubwa nchini Botswana, hatasahau jinsi madaktari wa Kundi la 17 la Timu ya Madaktari wa China walivyookoa maisha yake.

Kwa miaka mingi, Bosha, mwenye umri wa miaka 62, alikuwa akivumilia maumivu ya tumbo mara kwa mara, lakini awali aliyapuuza kuwa siyo jambo kubwa. Juni mwaka huu, baada ya kutembelea zahanati ya mtaani kwake, alipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Nyangabgwe iliyopo Francistown, ambako aligundulika kuwa na mawe kwenye figo.

"Mawe kwenye figo yalisababisha maumivu yasiyovumilika kwa miaka mingi," Bosha ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua pembeni ya kitanda chake, kufuatia upasuaji wa laparoscopic uliofaulu katika hospitali hiyo. Mama huyo wa watoto wawili, Bosha awali alifadhaika aliposhauriwa kufanyiwa upasuaji, kwani kwa muda mrefu alikuwa akihofia kufanyiwa upasuaji wenye majeraha makubwa na maumivu baada ya upasuaji huo.

Kwa bahati nzuri, matibabu ya Bosha yalikutana na kuwasili kwa Kundi la 17 la Timu ya Madaktari wa China, ambalo lilijumuisha Hu Minxiong, daktari wa mfumo wa mkojo aliyebobea katika kutibu maumivu ya tumbo yanayohusiana na mawe kwenye figo. Akiwa na utaalam wa upasuaji wa tumbo usio na maumivu sana na kuwa jeraha ndogo tu (laparoscopic surgery), Hu alianza haraka kusaidia wagonjwa waliohitaji mbinu hiyo.

"Sitasahau kamwe jinsi madaktari wa Kundi la 17 la Timu ya Madaktari wa China walivyoniokoa kutokana na uchungu wa miaka mingi," amesema Bosha mwenye kutabasamu, ambaye sasa ni mnufaika wa tano wa upasuaji huo ambao hauleti maumivu sana. Upasuaji wake huo, uliofanywa Oktoba, ulichukua dakika 90 tu, muda mfupi zaidi kuliko upasuaji wa kawaida wenye majeraha makubwa.

Kama mkulima mdogo, maumivu hayo ya tumbo yalikuwa yamemzuia Bosha kutunza mazao yake. "Sasa naweza kulima bila kusita," amesema. "Madaktari wa China wamenipa maisha mapya. Maumivu yalitoweka saa chache baada ya upasuaji."

Licha ya uzoefu mdogo wa Hospitali ya Rufaa ya Nyangabgwe katika upasuaji wa aina hiyo, madaktari wa China walishirikiana vilivyo na wenzao wenyeji kufanya upasuaji huo wa Bosha katika muda wa chini ya saa mbili, na kupongezwa na wenzao wa Botswana.

"Utaratibu huo ni wenye maumivu madogo, ukisababisha kutokwa na damu kidogo na kupona haraka," Hu ameelezea, akibainisha kuwa wenyeji wengi sasa wanachagua upasuaji huo.

Tangu Mwaka 1981, China imetuma timu 17 za madaktari watapao wafanyakazi wa afya 557 kwenda Botswana, wakitoa huduma za kliniki kwa wagonjwa zaidi ya milioni 2 katika kipindi cha miaka 43 iliyopita.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha