

Lugha Nyingine
Idadi ya vifo katika ajali ya barabarani nchini Ethiopia yafikia 71
Picha hii iliyopigwa Desemba 29, 2024 ikionyesha eneo la ajali ya barabarani katika Mkoa wa Sidama, Ethiopia. (Ofisi ya Kitaifa ya Afya ya Mkoa wa Sidama/ kupitia Xinhua)
ADDIS ABABA - Watu 71 wamefariki dunia siku ya Jumapili wakati lori lililokuwa limebeba abiria lilipoanguka kwenye mto katika Mkoa wa Sidama, kusini mwa Ethiopia, imesema kamisheni ya polisi ya mkoa huo, ambapo ajali hiyo imetokea wakati lori hilo lilipokuwa likisafiri kutokea Bona kwenda Bensa na kusababisha vifo hivyo vya wanaume 68 na wanawake watatu.
Katika taarifa ya awali iliripotiwa kuwa watu zaidi ya 60 wamefariki dunia kwenye ajali hiyo na kwamba majeruhi wamepatiwa matibabu kwenye hospitali zilizoko jirani na eneo la ajali.
Licha ya kiwango cha chini cha umiliki wa gari kwa kila mtu, ajali mbaya za barabarani ni za kawaida nchini Ethiopia. Hali mbaya ya barabara, kuendesha gari bila uangalifu, mfumo mbovu wa utoaji leseni, na uzembe wa usimamizi wa utekelezaji wa kanuni za usalama ni miongoni mwa sababu kuu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma