Ripoti maalumu ya mwishoni mwa mwaka: Afrika iliyoamka yaungana mikono na Nchi za Kusini kuendeleza maendeleo ya kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 31, 2024

Treni ya SGR inayotumia umeme ikiwa imesimama kwenye Stesheni ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Agosti 1, 2024. (Picha na Emmanuel Herman/Xinhua)

Treni ya SGR inayotumia umeme ikiwa imesimama kwenye Stesheni ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Agosti 1, 2024. (Picha na Emmanuel Herman/Xinhua)

NAIROBI, Desemba 28 (Xinhua) -- Katika mwaka wa 2024, Afrika imechukua nafasi muhimu katika ajenda ya maendeleo ya kimataifa, ikionyesha uhimilivu wa bara hilo na uhusiano wake wa kina na Nchi za Kusini katika jumuiya ya kimataifa.

Kuanzia Mkutano wa 19 wa Vuguvugu la Kutofungamana na Upande Wowote (NAM) na Mkutano wa 3 wa Nchi za Kusini uliofanyika Uganda hadi Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), Afrika imeonyesha dhamira na uwezo wake wa kuunganisha nchi za Kusini katika kutimiza maendeleo ya pamoja na kufanikisha kujenga mambo ya kisasa.

Kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Afrika ni miongoni mwa maeneo yaliyokua kwa kasi zaidi katika uchumi wa dunia mwaka 2024. Katikati ya mabadiliko ya haraka na makubwa duniani, uwezo na uhai wa bara hilo kubwa umeimarisha nafasi yake kama mdau muhimu katika kuunda mustakabali wa baadaye.

Picha hii iliyopigwa Juni 2, 2024 ikionesha muonekano wa mtaa karibu na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) iliyopo eneo la kati la kibiashara la Abidjan, Mji Mkuu wa Kiuchumi wa Cote d'Ivoire. Benki hiyo Mei 30 ilizindua mpango mkakati wake wa miaka 10 unaoeleza kwa namna gani benki hiyo mkopeshaji wa Afrika itaunga mkono bara hilo kuharakisha ukuaji jumuishi wa kijani na uchumi himilivu. (Picha na Laurent Idibouo/Xinhua)

Injini ya Ukuaji ya Siku za Baadaye

Katika medani ya kimataifa yenye changamano na kubadilika, mataifa ya Afrika yanatafuta maendeleo ya kujitegemea kupitia ujumuishaji wa kikanda.

Kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, ukuaji wa uchumi wa Afrika unatarajiwa kupanda tena hadi asilimia 3.7 mwaka 2024, ukizidi wastani wa kimataifa, na kufikia asilimia 4.3 mwaka 2025, ikilifanya bara hilo kuwa eneo la pili kwa ukuaji wa kasi duniani baada ya Asia.

Nchi nyingi za Afrika zimefanya chaguzi mwaka huu. Kuanzia Visiwa vya Comoro katika Afrika Mashariki hadi Senegal katika Afrika Magharibi, chaguzi nyingi zimefanyika kwa utulivu na utaratibu. Serikali mpya zimeweka maendeleo ya kiuchumi kuwa kipaumbele katika ajenda zao, zikitambua kwamba kujitegemea ni muhimu katika kupata nafasi ya ushindani katika medani ya kimataifa.

Kwa muktadha huu, nchi za Afrika zinaongeza kasi ya utekelezaji wa Mkataba wa Eneo la Biashara Huria Barani Afrika (AfCFTA). Mkataba huo umeanza kutekelezwa katika mataifa kadhaa, yakiwemo Afrika Kusini, Ghana na Kenya. Kwa mujibu wa ripoti ya Al-Mal News, gazeti la kila siku la Misri, biashara ndani ya bara inatarajiwa kukua kutoka dola bilioni 192.2 za Kimarekani mwaka 2023 hadi dola bilioni 520 ifikapo mwaka 2030 kufuatia uzinduzi wa AfCFTA.

Benki ya Dunia inakadiria kwamba AfCFTA inaweza kuongeza mapato ya bara hilo kwa asilimia 7 ifikapo mwaka 2035 na kuondoa watu milioni 30 kutoka katika umasikini uliokithiri.

Picha hii iliyopigwa Februari 17, 2024 ikionesha muonekano wa Mkutano wa Kawaida wa 37 wa Baraza Kuu la Viongozi wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Michael Tewelde)

Kuibuka kwa Nguvu ya Afrika

Mwaka 2024, Afrika imethibitisha tena dhamira yake thabiti ya kujenga mfumo wa kimataifa wenye haki na usawa zaidi. Hili linaonekana katika utetezi wake wa mageuzi katika utawala wa kimataifa, juhudi za kupatanisha migogoro ya siasa za kijiografia, na maendeleo katika kuhamia nishati mbadala.

Januari 1, Misri na Ethiopia zilijiunga rasmi na BRICS, ikiashiria kuongezwa kwa uwepo wa Afrika kwenye ushirikiano wa BRICS baada ya ushiriki wa Afrika Kusini.

Mwezi Novemba, Umoja wa Afrika (AU) ulishiriki kama mwanachama kamili katika mkutano wa kilele wa G20 kwa mara ya kwanza, ukijiunga na wengine kutoa wito wa kujengwa mfumo wa fedha wa kimataifa wenye haki zaidi, kutetea unafuu wa madeni, na kulinda maslahi ya nchi zinazoendelea. Desemba 1, Afrika Kusini ilichukua urais wa G20, na kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kushika nafasi hiyo. Kaulimbiu ya urais wake, "Mshikamano, Usawa, na Uendelevu," inaonyesha maono ya kipekee ya Afrika kwa ajili ya utawala wa kimataifa wa siku zijazo.

Wachambuzi wamesema kuwa Afrika inatathmini upya mwelekeo wake wa maendeleo, ikitafuta kujinasua kutoka kwenye vikwazo vya miundo ya maendeleo ya Magharibi na kujizatiti kwa kujitegemea kisiasa, kiuchumi, na kitamaduni.

Rais Xi Jinping wa China akihudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika 2024 (FOCAC) na kutoa hotuba muhimu kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

Juhudi za pamoja Kuelekea Maendeleo ya Kisasa

Mwezi Septemba, Mkutano wa FOCAC uliofanyika Beijing ulifikia hatua nyingine muhimu ya kihistoria katika uhusiano kati ya China na Afrika na kwa Nchi za Kusini kwa ujumla. China na Afrika ziliahidi kushikana mikono kutekeleza hatua 10 za ushirikiano ili kuendeleza maendeleo ya kisasa.

Mwezi Novemba, Maonesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) mjini Shanghai yalionesha bidhaa mbalimbali kutoka Afrika, zikiwemo parachichi za Afrika Kusini, asali ya Tanzania, na sukari ya Mauritius, ambazo zilionyeshwa kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Kuanzia Desemba 1, China imezipa nchi zzilizo za nyuma kimaendeleo ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia nayo, yakiwemo mataifa 33 ya Afrika, utozaji ushuru sifuri kwa asilimia 100 kwa bidhaa zao, na kuwa nchi kubwa inayoendelea ya kwanza na ya kwanza yenye uchumi mkubwa kuchukua hatua kama hiyo.

Mwezi Machi mwaka huu, wasomi wa China na Afrika walitoa kwa pamoja Azimio la Makubaliano ya Dar es Salaam kati ya China na Afrika, likisisitiza makubaliano kati ya Nchi za Kusini kuhusu njia na falsafa ya maendeleo.

(Makala hii imetafsiriwa kutoka makala ya Kiingereza ya Xinhua.)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha