Uhusiano kati ya China na Afrika waendelea kuzaa matunda katika mwaka 2024

(CRI Online) Januari 01, 2025

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema uhusiano kati ya China na Afrika uliendelea kuzaa matunda mwaka 2024 katika hali tete na yenye misukosuko mingi ya kimataifa.

Akiulizwa kuhusu ni mambo gani muhimu kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika kwa mwaka 2024 na mustakabali wa uhusiano wa pande hizo mbili kwenye mwaka 2025 siku ya Jumanne kwenye mkutano wa kila siku na waandishi wa habari, Bi. Mao Ning alikumbusha kuwa wageni takriban 6000 wa ndani na nje ya China walishiriki kwenye Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Septemba mjini Beijing, wakiwemo viongozi wa nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Aidha uhusiano wa pande mbili kati ya China na nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China umeinuliwa na kuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote katika zama mpya.

Kwa kutazamia mwaka 2025, Bi. Mao amesema China itaendelea kutekeleza matokeo ya Mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika Beijing na makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa China na Afrika, na kuongeza kuwa China itashirikiana na nchi za Afrika ili kuoaisha sera na mikakati ya maendeleo, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni na kati ya watu na watu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha