

Lugha Nyingine
SADC yahimiza kukomesha uhasama mara moja nchini Msumbiji
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imetoa wito wa kukomesha uhasama mara moja nchini Msumbiji, na kutandika njia ya mazungumzo ya kutatua mgogoro nchini humo.
Kwenye taarifa iliyotolewa na sekretarieti ya SADC siku ya Jumanne, Rais wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwenye SADC Samia Suluhu Hassan alisema SADC inatoa wito kwa pande zote kujizuia na vitendo vitakavyozidisha vurugu na mgogoro. SADC imesisitiza umuhimu wa kufanya mazungumzo ya amani na ya kiujenzi kuwa njia ya kwanza katika kutatua mgogoro.
Rais Samia ameongeza kuwa SADC ina wasiwasi mkubwa juu ya vifo, majeruhi na uharibifu kwa mali binafsi na miundombinu ya umma nchini Msumbiji, akisisitiza kuwa hali ya sasa pia inailetea nchi hiyo changamoto kubwa ya kiuchumi, ikisumbua biashara ya nje ya nchi, na kuzuia usafiri wa watu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma