Ligi kuu ya Vijijni ya China yaanzisha mualiko wa soka na Ethiopia

(CRI Online) Januari 01, 2025

Mechi ya kirafiki kati ya timu ya vijana wapenda soka kutoka Ethiopia walioalikwa na wenzao wa China ilifanyika Jumanne usiku katika wilaya ya Rongjiang, kusini magharibi mwa mkoa wa Guizhou nchini China.

Wilaya ya Rongjiang, mahali palipoasisiwa Ligi Kuu ya Vijiji ya Guizhou, ambayo pia inajulikana kama "Cun Chao," imepata umaarufu ndani na nje ya China kutokana na mapenzi ya wenyeji kwa soka na tamaduni tajiri za kikabila za eneo hilo. Wakati wa mapumziko, timu ya Ethiopia ilifanya maonesho ya kitamaduni kwa kutumbuiza kwa ngoma na muziki unaowakilisha mataifa yao tofauti.

Naibu mkuu wa wilaya ya Rongjiang, Chen Xuemin, alisema anaamini kuwa mechi hiyo inaweza kukuza mawasiliano na maelewano kati ya vijana kutoka nchi hizo mbili na kuimarisha urafiki kati ya China na Afrika.

Ikiwa imeanzishwa mwaka 2023, Ligi kuu ya Vijijini ya Guizhou imevutia zaidi ya mashabiki 1,100 wa soka kutoka zaidi ya nchi na kanda 50, zikiwemo Ufaransa, Liberia na Marekani, kushiriki katika mechi za kirafiki mjini Rongjiang.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha