Kampuni ya magari ya BYD ya China yaripoti kuongezeka kwa mauzo ya magari ya nishati mpya mwaka 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 02, 2025

Picha hii ikionyesha gari aina ya Yangwang U7 ya Kampuni ya Magari ya BYD katika Maonyesho ya 22 ya Kimataifa ya Magari ya Guangzhou kwenye Jumba la Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China mjini Guangzhou, Mkoani Guangdong, Kusini mwa China, Novemba 15, 2024. (Xinhua/Deng Hua)

Picha hii ikionyesha gari aina ya Yangwang U7 ya Kampuni ya Magari ya BYD katika Maonyesho ya 22 ya Kimataifa ya Magari ya Guangzhou kwenye Jumba la Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China mjini Guangzhou, Mkoani Guangdong, Kusini mwa China, Novemba 15, 2024. (Xinhua/Deng Hua)

SHENZHEN - Kampuni ya magari ya BYD ya China imeshuhudia mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya (NEV) yakipanda kwa asilimia 41.26 mwaka hadi mwaka kufikia zaidi ya milioni 4.27 mwaka 2024, kampuni hiyo imesema katika ripoti yake kwenye Soko la Hisa la Shenzhen jana Jumatano.

Magari ya abiria milioni 4.25 ya kampuni hiyo yameuzwa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 41.07 kuliko mwaka uliopita, hali ambayo imeongoza mauzo yake ya NEV.

Kwa mujibu wa idadi hiyo, magari yanayotumia umeme kikamilifu yalichukua zaidi ya magari milioni 1.76, ikiongezeka kwa asilimia 12.08 mwaka hadi mwaka, wakati magari ya nishati mchangayiko ya kuchaji yaliongezeka kwa asilimia 72.83 hadi kufikia karibu milioni 2.49.

Wakati huo huo, mauzo ya nje ya nchi ya magari ya abiria yanayotumia nishati mpya ya kampuni hiyo yalikua kwa asilimia 71.9 mwaka hadi mwaka hadi kufikia 417,200 mwaka jana, ikionyesha upanuzi wa kampuni hiyo katika masoko ya kimataifa.

BYD ni moja ya kampuni zinazozalisha magari yanayotumia nishati mpyanchini China, ambayo inauza idadi kubwa ya magari duniani, ikiendelea na kubadili muundo wake wa teknolojia kuwa ya kijani.

Kampuni za kuzalisha magari za China ziliuza magari yanayotumia nishati mpya zaidi ya milioni 11.26 katika miezi 11 ya kwanza ya mwaka 2024, ikiongezeka kwa asilimia 35.6 kuliko mwaka uliopita, kwa mujibu wa Jumuiya ya Wazalishaji Magari ya China.

Huku kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kukiwa kipaumbele cha kimataifa, magari yanayotumia nishati mpya yamebeba jukumu muhimu katika kupunguza utoaji wa kaboni katika sekta ya usafirishaji. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Nishati, mauzo ya kimataifa ya magari yanayotumia nishati mpya yanahitaji kufikia magari milioni 45 ifikapo mwaka 2030 ili kufikia malengo ya kusawazisha hewa ya kaboni.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha