China yapeleka msaada wa dharura kwa Vanuatu iliyokumbwa na tetemeko la ardhi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 02, 2025

Vifaa vya msaada wa dharura vyenye maandishi ya "Msaada wa China" vikipakiwa ndani ya ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shenzhen Baoan mjini Shenzhen, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Januari 1, 2025. (Xinhua/Liang Xu)

Vifaa vya msaada wa dharura vyenye maandishi ya "Msaada wa China" vikipakiwa ndani ya ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shenzhen Baoan mjini Shenzhen, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Januari 1, 2025. (Xinhua/Liang Xu)

SHENZHEN - Shehena ya vifaa vya msaada wa dharura imeondoka jana Jumatano jioni kutoka mji wa kusini mwa China wa Shenzhen hadi Port Vila, mji mkuu wa Vanuatu, kuunga mkono juhudi za uokoaji wa tetemeko la ardhi katika nchi hiyo ya kisiwa cha Pasifiki.

Ndege hiyo, ikiwa imebeba vifaa muhimu vikiwemo mahema, vitanda vya kukunjika, vifaa vya kusafisha maji, taa zinazotumia nishati ya jua, vyakula vya dharura na vifaa tiba, iliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shenzhen Baoan majira saa 1:18 jioni (Saa za Beijing). Ilikuwa ikitarajiwa kuwasili Port Vila majira ya saa 10:45 alfajiri, leo Alhamisi (kwa saa za huko), kwa mujibu wa mamlaka za usafiri wa anga.

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.3 katika kipimo cha Richta lilipiga Port Vila Desemba 17, likisababisha vifo na majeruhi wengi na uharibifu mkubwa.

Serikali ya China imetoa msaada wa dharura wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 1, Li Ming, msemaji wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa la China, alitangaza wiki iliyopita.

Kutokana na ombi la serikali ya Vanuatu, China imetuma wataalam wanne wa uhandisi kusaidia kukabiliana na tetemeko hilo la ardhi nchini humo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning alisema Jumatatu.

"Hii ni mara ya kwanza kwa China kutuma timu ya dharura ya tathmini baada ya maafa katika nchi ya kisiwa cha Pasifiki, ikiwa na matumaini ya kutoa mchango kwa ajili ya ukarabati wa Vanuatu," Mao alisema kwenye mkutano huo na waandishi wa habari.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha