

Lugha Nyingine
Mikono midogo, ndoto kubwa: Vijana wa Namibia wapata masikilizano katika muziki wa okestra
Vijana wakipiga ala za muziki kwenye Orkestra ya Vijana ya Namibia mjini Windhoek, Namibia, Desemba 15, 2024. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)
WINDHOEK - Kwa mipigo maridadi ya fidla yake, Twani Fredericks mwenye umri wa miaka 18 alijaza darasa la Vijana wa Orchestra ya Namibia (YONA) kwa muziki za kuvutia. Uzoefu wake wa kutumia ala siyo tu unahusu shauku yake kubwa bali pia ustahimilivu unaohitajika katika kutimiza ndoto yake katika nchi ambayo ina fursa chache za kusoma muziki wa okestra.
"Kujifunza muziki wa okestra hapa kumebadili mawazo yangu. Kupiga fidla huleta tulivu moyoni mwangu. Ninaipenda," amesema Fredericks, ambaye alianza safari yake ya muziki akiwa na umri wa miaka 11.
Fredericks ni mmoja wa wanufaika wengi wa YONA, ambayo ilianzishwa mwaka 2016 ili kukuza vipaji vya kisanii mjini Windhoek, mji mkuu wa Namibia. Tangu kuanzishwa kwake, programu hiyo imewezesha watoto zaidi ya 600, ikishughulikia tatizo la pengo la Namibia katika kutoa mafunzo kwa wanamuziki wa okestra.
"Dhamira yetu ni kuziba mapengo na kuhamasisha matumaini, kuwezesha watoto kujenga maisha bora ya baadaye," amesema Gretel Coetzee, mkurugenzi ambaye pia ni mwanzilishi mwenza wa YONA. Amesema kuwa orkestra nchini Namibia hapo awali zilitegemea wanamuziki kutoka nchi jirani, hatua ambayo YONA inaibadilika polepole kwa kukuza vipaji vya ndani.
Waziri wa Elimu, Sanaa na Utamaduni wa Namibia Ester Anna Nghipondoka amesema programu kama YONA ni muhimu katika kukuza vipaji vya vijana licha ya rasilimali chache, akisisitiza kuwa programu hizo zina jukumu muhimu katika kufungua uwezo na kuunda mustakabali wa vijana.
Kile kilichoanza na watoto 25 kimechanua na kuwa programu inayostawi, ikichukua wanafunzi wapatao 200 kwa mwaka kwenye kituo chake kikuu katika eneo la kati la kibiashara la Windhoek na vituo vingine viwili katika kitongoji cha Katutura.
"Tulipoanzisha masomo ya fidla kwa mara ya kwanza mwaka 2017, watoto 25 walipaswa kutumia pamoja ala nne tu kujifunza moja baada ya mwingine," Coetzee amekumbushia.
YONA sasa inatoa masomo katika ngazi tatu, kutoka upigaji okestra na kwaya wa awali hadi vikundi vyenye ujuzi wa hali ya juu vya kupiga simfoni. Aina mbalimbali za ala pia zimeongezeka na kuwa na filimbi, piano, klarinet, na oboe, ikioonyesha shauku inayoongezeka miongoni mwa watoto.
Ujumuishaji ni msingi wa falsafa ya YONA. Wakati chuo hicho kinatoza ada za kawaida, asilimia takriban 80 ya wanafunzi hupokea ufadhili kutoka mashirika kama vile Baraza la Sanaa la Taifa la Namibia. Ufadhili huo unagharimia masomo, usafiri, na chakula, kuhakikisha kwamba elimu ya muziki wa okestra inaendelea kupatikana kwa watoto kutoka hali mbalimbali.
"Hii inahakikisha kwamba elimu ya muziki wa okestra inapatikana kwa watoto wengi iwezekanavyo, ikiongeza ujumuishaji huku ikitumia nguvu ya muziki kujenga maisha ya vijana katika miaka yao ya kukua," Coetzee amesema.
Watoto wakicheza ala za muziki katika Orchestra ya Vijana ya Namibia mjini Windhoek, Namibia, Desemba 15, 2024. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma