

Lugha Nyingine
Rais wa Kenya asema mageuzi yanatarajia kuhimiza uchumi mwaka 2025
Rais William Ruto wa Kenya Jumanne amesema mageuzi yanayofanywa na serikali yake yanatarajiwa kuhimiza zaidi uchumi, kuongeza fursa za ajira kwa vijana, na kuongeza mapato ya wakulima na wajasiriamali.
Akitoa hotuba ya mwisho wa mwaka huko Kisii, magharibi mwa Kenya, Rais Ruto amesema serikali imefanikiwa kuweka msingi imara katika kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hiyo katika mwaka 2025.
Amehimiza Wakenya kukaribisha mwaka mpya kwa imani, matumaini na dhamira ili kutimiza malengo ya Kenya.
Ameongeza kuwa maendeleo ya Kenya yanaifanya nchi hiyo kuwa katika njia ya ukuaji endelevu na wa kasi ambapo Pato la Taifa la Kenya kwa mwaka 2023 limeongezeka kwa asilimia 5.6, hali ambayo inaifanya Kenya kuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi duniani.
Inakadiriwa kuwa uwekezaji mwingi utapatikana mwaka 2025, ambao utahimiza kupanuka kwa sekta ya viwanda na kuongeza uuzaji nje wa bidhaa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma