Msukosuko wa maji katika Port Sudan wazidi kuongezeka baada ya bwawa kupasuka na kuwepo kwa wimbi la wakimbizi

(CRI Online) Januari 02, 2025

Wakaazi wa Port Sudan, mji mkuu wa Jimbo la Bahari ya Sham mashariki mwa Sudan, wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji ya kunywa kufuatia kupasuka kwa kingo za Bwawa la Arbaat mwezi Agosti na wimbi la watu wanaokimbia makazi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea.

Mikokoteni inayokokotwa na wanyama imeonekana tena katika mitaa ya mji huo wa pwani, ikisafirisha maji ya kunywa kutoka vyanzo vichache vilivyoko umbali wa kilomita 20 kaskazini mwa Bandari ya Sudan hadi kwenye kaya na maeneo ya biashara.

Kwa mujibu wa mbeba maji mwenyeji Mustafa Hamad, kupasuka kwa kingo za Bwawa la Arbaat, ambalo hapo awali lilikuwa chanzo kikuu cha maji safi katika mji huo, kumesababisha bei ya maji kupanda zaidi ya mara mbili.

Amesema, pipa la ujazo wa lita 220 sasa linagharimu pauni 25,000 za Sudan (kama dola 10 za Kimarekani sokoni).

Msukosuko huo umelazimu baadhi ya wakazi kutumia maji ya chumvi na machafu kama njia mbadala na kusababisha matatizo ya kiafya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha