Rais Xi na mke wake wawatumia kadi ya Mwaka Mpya wawakilishi wa walimu na wanafunzi wa sekondari ya Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan, Jumatano waliwatumia kadi ya Mwaka Mpya wawakilishi wa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari za Jimbo la Washington la Marekani, wakitoa salamu zao za Mwaka Mpya

Katika kadi hiyo, Rais Xi na mkewe Peng wamesema mwaka 2025 ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupata ushindi wa Vita vya Watu wa China vya kupambana na uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya kupambana na Ufashisti.

Wamesema, kaika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, China na Marekani zilipambana na wavamizi pamoja kwa ajili ya amani na haki, na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili ulijaribiwa katika vita vya kumwaga damu na vya moto, na umeimarishwa siku hadi siku.

Wanandoa hao wameeleza matumaini yao kuwa vijana wa China na Marekani wataendelea kushiriki katika mpango wa China wa kuwaalika vijana 50,000 wa Marekani kuja China kufanya mawasiliano na kusoma ndani ya miaka mitano, kuongeza maingiliano na michangamano, kuongeza maelewano, na kuenzi urafiki wa jadi, ili kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano wa China na Marekani na amani ya Dunia.

Awali, Shirika la Mawasiliano ya Vijana na Wanafunzi wa Marekani na China, na wawakilishi wa walimu na wanafunzi wa Sekondari ya Juu ya Lincoln na Sekondari ya Juu ya Stadium, ambao walitembelea China kupitia mpango huo wa China walituma kadi ya Mwaka Mpya kwa Rais Xi na mkewe Peng na watu wa China. Walimu na wanafunzi zaidi ya 100 walitia saini kwenye kadi hiyo.

Waliandika kwa Lugha ya Kichina kwenye kadi hiyo kutoa salamu za Mwaka Mpya na kutakia urafiki udumu milele kati ya China na Marekani. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha