Lugha Nyingine
China yaimarisha kazi husika ya nchi mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya Ushirikiano ya Shanghai
BEIJING – Msemaji wa wizara ya mambo ya China amesema Alhamisi kwamba, China siku zote hizi inaharakisha kazi husika ya nchi mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) katika mwaka 2025.
Msemaji huyo amesema, China ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya Usirikiano ya Shanghai mwaka 2025, itaandaa mkutano wa kilele wa SCO ambao unaangazia urafiki, mshikamano na matunda kemkem, pamoja na mikutano zaidi ya 40 ya kitaasisi.
Msemaji huyo ameongeza kuwa, shughuli zinazohusu mada kama vile vyama vya siasa, kupunguza umaskini, maendeleo endelevu, na mawasiliano ya kitamaduni kati ya watu na watu zitafanyika mwaka huu, pamoja na maonyesho ya uwekezaji na biashara, tamasha la filamu na shughuli za michezo ya sanaa.
China pia imetangaza nembo ya nchi mwenyekiti wa zamu wa 2024-2025 SCO siku ya Alhamisi. Nembo hili limeonesha utamaduni wa China, na juu yake michoro ya mapambo ya jadi ya vyombo vya shaba nyeusi vya zama za kale za China inazunguka maneno ya kauli mbiu ya "Kushikilia Moyo wa Shanghai: SCO Inasonga Mbele" kwa Lugha ya Kichina, Kirusi na Kiingereza.
Nembo ya nchi mwenyekiti wa zamu wa 2024-2025 SCO (Picha/Xinhua)
Msemaji huyo amesema kuwa China ikiwa nchi mwenyekiti wa zama, kazi yake muhimu ni kufanya vitendo vya kufuata hali halisi zaidi na kupatia maendeleo zaidi, kuinua hatua kwa hatua kiwango cha ushirikiano wa SCO katika sekta za siasa, usalama, uchumi na utamaduni, kukamilisha mfumo wa uendeshaji wa jumuiya hiyo, kujenga jumuiya ya SCO yenye mustakabali wa pamoja na kupanua uwezekano mpya wa maendeleo yenye manufaa kwa pande zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma