Kituo cha Utafiti wa Kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja chazinduliwa mjini Beijing

(CRI Online) Januari 03, 2025

Kituo cha Utafiti kuhusu mambo yanayohusiana na Ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja kimezinduliwa rasmi Alhamisi mjini Beijing.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alitoa hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo hicho katika Chuo Kikuu cha Mambo ya Kigeni cha China.

Wang amesema ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja ni fikra kuu iliyotolewa kwa mara ya kwanza na Rais Xi Jinping wa China, pia ni wazo kuu la Fikra ya Xi Jinping juu ya Diplomasia.

Huu ni mwitikio wa China juu ya suala la kujenga dunia ya aina gani na jinsi ya kujenga dunia hiyo” amesema Wang, huku akiongeza kuwa jambo hilo lina thamani kubwa ya kinadharia, umuhimu mkubwa kwa zama hii na ushawishi mkubwa kwa dunia.

Amesema kuwa, maono ya jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja yanaonyesha dhamira ya kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), kuendeleza desturi za utamaduni wa China, kuonyesha nguvu ya nadharia za kisayansi, na kueleza msimamo wa China juu ya kukabiliana na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita.

Wang amehimiza kituo hicho cha utafiti kutekeleza kwa umakini majukumu ya kujifunza, kueleza na kueneza Fikra ya Xi Jinping juu ya Diplomasia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha