

Lugha Nyingine
Uganda yasema ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kikanda unaendelea
Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda Ruth Nankabirwa amesema kuwa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi lenye urefu wa kilomita 1,443 kati ya Uganda na nchi jirani ya Tanzania unaendelea kama ulivyopangwa.
“Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) lenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.55 kati ya visima vya mafuta vya Albertine Graben magharibi mwa Uganda na bandari ya Tanga nchini Tanzania unaendelea vizuri” Nankabirwa amenukuliwa akisema.
Amesema, hadi sasa kilomita 1,100 za bomba zimeshajengwa na kufika Tanzania kati ya jumla ya kilomita 1,443 zinazotarajiwa. Kukamilika kwa mtambo wa kudhibiti moto nchini Tanzania na uwasilishaji wa laini ya mabomba yenye nyenzo za kuhimili joto ni hatua muhimu” amesema.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, mkandarasi wa ujenzi wa EACOP, kampuni ya Uhandisi wa Mabomba ya Mafuta ya China alianza kazi katika vituo vya pampu, kambi kuu, na maeneo ya mabomba nchini Uganda na Tanzania mwaka 2024.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma