Waziri wa Mambo ya Nje wa China kufanya ziara Namibia, Jamhuri ya Kongo, Chad, Nigeria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2025

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ameanza ziara nchini Namibia, Jamhuri ya Kongo, Chad na Nigeria kuanzia Januari 5 hadi Januari 11, kwa kufuata desturi ya waziri wa mambo ya nje wa China kufanya kwanza ziara Afrika katika ziara yake nje ya nchi mwanzoni mwa kila mwaka katika miaka 35 iliyopita, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning alitangaza Ijumaa.

Msemaji huyo amesema, Ziara hiyo ya Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), inalenga kuhimiza utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa Beijing, kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kufuata hali halisi katika sekta mbalimbali, na kuhimiza maendeleo endelevu na ya kina ya uhusiano kati ya China na Afrika.

Katika mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing mwaka jana, Rais Xi Jinping wa China alipendekeza kuwa uhusiano wa pande mbilimbili kati ya China na nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China upandishwe ngazi hadi kufikia ngazi ya uhusiano wa kimkakati, na sifa ya jumla ya uhusiano kati ya China na Afrika iinuliwe hadi kufikia ngazi ya jumuiya ya China na Afrika ya siku zote yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Msemaji huyo amesema, "Rais Xi pia alipendekeza kuwa China na Afrika zinapaswa kuendeleza kwa pamoja ujenzi wa mambo sita maalumu ya kisasa, na kuahidi kuwa China itashirikiana na Afrika katika kuhimiza pamoja mipango 10 ya utekelezaji ya ujenzi wa mambo ya kisasa, ambayo imepokea mwitikio mzuri kutoka kwa upande wa Afrika".

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha