

Lugha Nyingine
Wataalam wasema safari nyingi za abiria zinazovunja rekodi zinaonyesha kuongezeka kwa nguvu za uchumi wa China
Abiria wakisubiri ndani ya treni ya mwendokasi kuelekea Beijing kwenye Stesheni ya Reli ya Tianjin mjini Tianjin, kaskazini mwa China, Desemba 10, 2024. (Xinhua/Li Ran)
BEIJING - China imeshuhudia ongezeko kubwa la safari za reli na anga mwaka 2024, lililochochewa na kushamiri kwa shughuli za kiuchumi na matumizi mengi ya watumiaji ambapo mtandao wa reli wa nchi hiyo ulishughulikia safari za abiria bilioni 4.08 mwaka wa 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.8 mwaka hadi mwaka, Shirika la Kundi la Kampuni za Reli la China limesema.
Vile vile, takwimu mpya zilizotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC) zinaonyesha kuwa safari za abiria za anga zinakadiriwa kufikia milioni 730 mwaka wa 2024, kiasi ambacho ni ongezeko la asilimia 18 mwaka hadi mwaka.
“Ikiwa injini ya ukuaji wa uchumi, takwimu za safari zinazovunja rekodi zinaonyesha kuongezeka kwa madhubuti kwa nia wa matumizi katika manunuzi wa China” Xu Hong, Mkuu wa chuo cha Utalii na Usimamizi wa Huduma katika Chuo Kikuu cha Nankai cha China amesema.
Amebainisha kuwa, ongezeko hilo kubwa kwa kiasi fulani limetokana na kuongezeka kwa mahitaji ya kusafiri kwa burudani, huku sekta ya utalii imekuwa kama sekta inayostawi ya uchumi wa China mwaka 2024.
Katika robo tatu za kwanza za mwaka jana, China iliripoti safari za ndani bilioni 4.24, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.3 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Thamani ya jumla ya matumizi katika manunuzi ya watalii wa ndani ilifikia yuan trilioni 4.35 (dola za kimarekani kama bilioni 605), ambayo ni ongezeko la asilimia 17.9 mwaka hadi mwaka.
Kutokana na kuboreshwa kwa miundombinu, maeneo mbalimbali na vivutio vya watalii visivyojulikana yanafikiwa kwa urahisi zaidi, mwelekeo wa kusafiri katika maeneo ya utalii yasiyo kawaida umeimarika, ukivuta watalii kujionea mambo mapya na mazuri.
Lu Wei, mtafiti katika Akademia ya Utafiti wa Uchumi Mkuu ya China, amebainisha kuwa maeneo ya ngazi ya chini yenye viwanja vya ndege yamezidi kuwa maarufu miongoni mwa watalii wa China.
Zaidi ya pilikapilika na kushamiri kwa soko la utalii wa ndani, safari za watalii wa kimataifa pia zilistawi mwaka jana, huku kukiwa na ongezeko la watalii wanaoingia China na wanaosafiri kwenda ng’ambo.
Kushamiri huko kwa safari za kitalii nchini China, kulikochochewa na upanuzi wa nchi hiyo wa sera ya msamaha wa visa, kumesababisha watalii wa kimataifa kumiminika nchini humo ili kujionea mchanganyiko wake wa jadi za historia zaidi ya miaka 100 na teknolojia ya kisasa. Mazingira ya malipo yaliyoboreshwa, alama za maelekezo mbalimbali kwa lugha mbili na hatua nyingine za uungaji mkono zimefanya safari nchini China kuwa rahisi zaidi kwa watalii wa kigeni.
"Kustawi kwa soko la watalii wanaoingia kunalingana vyema na mtazamo wa China katika kuchochea mahitaji," Xu amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma