Rais wa Tanzania Zanzibar apongeza kampuni ya China kwa ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi

(CRI Online) Januari 06, 2025

Rais wa Tanzania Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Kampuni ya Uhandisi wa Reli ya Jianchang (CRJE) ya China tawi la Afrika Mashariki, kwa ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi iliyoko Kijangwani kisiwani Unguja.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa stendi hiyo, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 61 tangu kutokea Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari, Rais Mwinyi amesema mradi huo si tu utaboresha usafiri kwa wakazi, bali pia utakuza uchumi wa visiwani humo, kuleta urahisi zaidi kwa ujumla na kuingiza uhai wa kiuchumi katika visiwa hivyo.

Meneja wa CRJE tawi la Zanzibar Gao Yuqi amesema, kituo hicho ambacho ni cha kwanza cha kisasa cha mabasi visiwani Zanzibar, kinajumuisha maeneo matatu ya abiria kusubiria mabasi, na sehemu zaidi ya 70 za maegesho ya mabasi, na maduka 128.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha