

Lugha Nyingine
Ethiopia yaisifu kampuni ya China kwa mchango wake katika utoaji ajira na ujenzi wa uwezo
Serikali ya Ethiopia imeipongeza kampuni ya Kundi la Kampuni za Huajian ya China kwa mchango wake mkubwa katika uwekezaji wake nchini Ethiopia ambao umetoa ajira na ujenzi wa uwezo kwa wenyeji.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Maeneo Maalum ya Viwanda nchini Ethiopia (IPDC) siku ya Jumamosi imeisifu kampuni hiyo kwa kutoa nafasi za ajira zilizonufaisha maelfu ya Waethiopia, na pia mchango wa kampuni hiyo katika kuhamisha teknolojia, maarifa, na ujuzi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa IPDC Fisseha Yitagesu amesema wakati wa majadiliano na wawakilishi wa kampuni hiyo ya Huajian nchini Ethiopia, kwamba serikali ya Ethiopia imeendelea kuunga mkono uwekezaji wa sasa na ujao wa kampuni hiyo nchini humo.
Wakati wa majadiliano hayo, wawakilishi wa kampuni ya Huajian pia wameeleza shauku yao kubwa ya kuwekeza katika Eneo la Biashara Huria la Dire Dawa nchini Ethiopia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma