Watoto 98 wazaliwa siku ya mwaka mpya nchini Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2025

Picha hii iliyopigwa Oktoba 31, 2024 ikionyesha mwonekano wa Gaborone, Botswana. (Xinhua/Han Xu)

Picha hii iliyopigwa Oktoba 31, 2024 ikionyesha mwonekano wa Gaborone, Botswana. (Xinhua/Han Xu)

GABORONE - Watoto jumla ya 98 wamezaliwa nchini Botswana siku ya kwanza ya mwaka mpya Januari 1, Mwaka 2025, Wizara ya Afya ya Botswana imetangaza ikiongeza kuwa idadi hiyo ni ongezeko kubwa la kushangaza kuliko mwaka uliopita ambapo watoto 46 tu ndiyo walizaliwa siku hiyo.

Katika taarifa yake ya siku Ijumaa, wizara hiyo imesema kuwa wengi wa watoto hao wamezaliwa Gaborone, mji mkuu wa Botswana, ikifuatiwa na Francistown na Maun, miji mingine miwili mikubwa muhimu nchini humo.

Idadi ya watu wa Botswana iliyokadiriwa katika Sensa ya Watu na Nyumba za Kukaa ya mwaka 2022 ilikuwa watu 2,346,179, ambao waliongezwa kwa asilimia 15.9 kutoka 2,024,904 waliosajiliwa katika sensa ya mwaka 2011. Matokeo mapya ya sense yanaonyesha kuwa idadi ya watu katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, kama haiongezeki, na itachukua angalau miaka 58 ndipo itakapofikia zaidi ya watu milioni 4.

Rais wa Botswana Duma Boko hivi majuzi aliuambia mkutano wa mashauri ya umma mjini Mahalapye kwamba serikali mpya itaanzisha programu zinazolenga kuhimiza wenyeji kupata watoto zaidi. 

Picha hii iliyopigwa Oktoba 31, 2024 ikionyesha mwonekano wa machweo ya Gaborone, Botswana. (Xinhua/Han Xu)

Picha hii iliyopigwa Oktoba 31, 2024 ikionyesha mwonekano wa machweo ya Gaborone, Botswana. (Xinhua/Han Xu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha