Tanzania yajiandaa kwa mkutano wa kilele wa nishati ili kuongeza upatikanaji wa umeme

(CRI Online) Januari 06, 2025

Mamlaka nchini Tanzania zimesema maandalizi ya Mkutano wa Kilele wa Nishati wa Viongozi Wakuu wa Serikali za Afrika uliopangwa kufanyika kuanzia tarehe 27 hadi 28 mwezi huu yanaendelea vizuri.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Pande Nyingi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Noel Kaganda amesema jijini Dar es Salaam kwamba, Tanzania ni mwandaaji mwenza wa mkutano huo, ambao utakutanisha wajumbe zaidi ya 1,500, wakiwemo wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika, Benki ya Maendeleo ya Afrika, na Benki ya Dunia.

Amesema mkutano huo utatumika kama jukwaa kwa serikali, viongozi wa sekta binafsi, washirika wa maendeleo na mashirika ya kijamii kuendeleza lengo la upatikanaji wa umeme kwa Waafrika milioni 300 ifikapo mwaka 2030.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha