

Lugha Nyingine
Watu 10 wauawa na wengine 30 kujeruhiwa katika shambulizi la anga nchini Sudan
(CRI Online) Januari 06, 2025
Kundi la kujitolea na Chumba cha Dharura lililoko Kusini mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum, na vyombo vya habari vya huko vimesema, watu takriban 10 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa katika shambulizi la anga lililotokea jana Jumapiki likilenga kituo cha Al-Sahrij, kusini mwa mji wa Khartoum.
Kundi hilo limesema, kituo cha Al-Sahrij kimeshambuliwa kwa mabomu mara tatu ndani ya mwezi mmoja, na kuongeza kuwa, eneo hilo lina msongamano mkubwa wa raia kwa kuwa kuna soko na migahawa mingi.
Bado hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma