

Lugha Nyingine
Marais wa China na Botswana watumiana salamu za pongezi juu ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China na Rais Duma Boko wa Botswana wametumiana salamu za pongezi jana siku ya Jumatatu kwa kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Rais Xi ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka 50 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, haijalishi jinsi gani hali ya kimataifa inavyobadilika, uhusiano kati ya China na Botswana siku zote umedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo, na nchi hizo mbili zimekuwa marafiki wazuri wanaotendeana kwa usawa na washirika wazuri wanaojiendeleza kwa pamoja.
Amesema anaamini kwamba mradi nchi hizo mbili zinashikilia urafiki, mshikamano na ushirikiano kwa dhati, njia ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Botswana hakika itakuwa pana zaidi, na mustakabali wa ushirikiano kati ya pande mbili hakika utakuwa mzuri zaidi.
“Mwaka 2025 ni mwaka wa mwanzo wa utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),” Rais Xi amesema.
Amesema kwa kusimama kwenye hatua mpya, angependa kushirikiana na rais Boko kwa ajili ya kuimarisha zaidi hali ya kuaminiana kisiasa, kuunga mkono kithabiti masuala makuu yanayofuatiliwa na pande mbili, kusongesha mbele kwa pamoja ujenzi wa mambo ya kisasa wa kila upande, na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa kimkakati na ushirikiano kati ya China na Botswana.
Rais Boko akipongeza maadhimisho hayo ya miaka 50 kama hatua muhimu katika uhusiano kati ya Botswana na China, ametoa shukurani za dhati kwa China kutokana na urafiki, mshikamano na ushirikiano mkubwa katika miaka hiyo 50 iliyopita.
Amesema Botswana imehamasishwa sana na mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyopatikana na China na kwamba anaamini ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili utaleta fursa kwa maendeleo jumuishi ya Botswana.
Akieleza uungaji mkono thabiti wa Botswana kwa sera ya kuwepo kwa China moja, Rais Boko amesema anatumai kuimarisha zaidi uhusiano kati ya Botswana na China unaojikita katika kuaminiana na kuheshimiana, na kutekeleza kwa pamoja matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Beijing wa FOCAC ili kupata maendeleo na ustawi wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma