China daima imedumisha ushirikiano wa kirafiki na Afrika: Msemaji Wizara ya Mambo ya Nje

(CRI Online) Januari 07, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Guo Jiakun amesema urafiki kati ya China na Afrika una historia ndefu, na Afrika inayokua itatoa mchango mkubwa zaidi kwa amani na maendeleo ya dunia.

Guo Jiakun amesema hayo jana Jumatatu alipokuwa akizungumzia ziara ya kwanza ya Waziri wa Mambo ya Nje ya China Wang Yi barani Afrika. Amesema katika ziara hiyo iliyoanza Januari 5 na inatarajiwa kumalizika Januari 11, Wang Yi atatembelea nchi nne za Afrika.

Bw. Guo Jiakun amesema, desturi ya ziara ya kwanza ya mwanzo wa mwaka ya waziri wa mambo ya nje wa China barani Afrika imedumu kwa miaka 35 mfululizo, ikidhihirisha kikamilifu urafiki wa jadi uliodumu kwa muda mrefu kati ya China na Afrika na ushirikiano thabiti wa kirafiki wa pande hizo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha