

Lugha Nyingine
China yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada wa kibinadamu kwa Sudan
(CRI Online) Januari 07, 2025
Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa jana Jumatatu kuendelea kuongeza msaada wa kibinadamu kwa Sudan.
Balozi Geng amehimiza Umoja wa Mataifa kuimarisha ushirikiano na pande mbalimbali ikiwemo serikali ya Sudan, ili kuhakikisha vifaa vya msaada vinaweza kuwafikia wahitaji, na kuleta matumaini kwa raia wa Sudan wanaokabiliwa na matatizo.
Balozi Geng ameongeza kuwa, msaada wa chakula uliotolewa na China umewasili nchini Sudan, na China itashirikiana na jumuiya ya kimataifa kuonesha umuhimu wa kiujenzi kwa Sudan kurudisha amani na utulivu mapema iwezakanavyo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma