Namibia na China zadhamiria kusukuma mbele zaidi ushirikiano wa kunufaishana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2025

WINDHOEK -Rais mteule wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah Jumatatu alikutana na Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) mjini Windhoek, mji mkuu wa Namibia.

Kwenye mkutano huo, Wang aliwasilisha salamu kutoka kwa Rais Xi Jinping wa China kwa Rais Ndaitwah, kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Namibia na kueleza kutakia Namibia kupata mafanikio makubwa katika ujenzi wa taifa.

Amesema mawaziri wa mambo ya nje wa China wameifanya Afrika kuwa kituo cha ziara zao za kwanza nje ya nchi mwanzoni mwa kila mwaka kwa miaka 35 mfululizo, desturi inayosisitiza namna ya kipekee ya kidiplomasia ya China.

Akibainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Namibia, Wang amesema ushirikiano kati ya pande mbili una fursa kubwa katika siku zijazo.

Amekumbushia mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wenye mafanikio uliofanyika Beijing mwaka jana wakati rais wa China alipotangaza mipango 10 ya ushirikiano ili kuhimiza kwa pamoja ujenzi wa mambo ya kisasa.

Wang ameelezea nia ya China ya kushirikiana na Namibia kuharakisha utekelezaji wa matokeo ya mkutano huo ili kuhakikisha upigaji hatua katika ushirikiano wao wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote.

“China itaendelea kuiunga mkono Namibia katika kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali yake ya kitaifa,” amesema Wang, akipongeza Namibia kushikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja.

Huku mwaka 2025 ukiadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, Wang ametoa wito wa kuwepo kwa uratibu imara zaidi wa kimkakati katika mambo ya pande nyingi ili kulinda maslahi ya pamoja ya Afrika na nchi zinazoendelea, huku zikishikilia haki na usawa wa kimataifa.

Kwa upande wake Rais mteule Ndaitwah amemwomba Wang kuwasilisha salamu zake za dhati kwa Rais Xi Jinping na shukrani kwa ujumbe wake wa pongezi baada ya uchaguzi wa rais wa Namibia.

Amekaribisha ziara ya Wang barani Afrika na nchini Namibia mwanzoni mwa mwaka mpya, akibainisha kuwa ni waziri wa mambo ya nje wa kwanza ambaye amekutana naye tangu alipochaguliwa kuwa rais, jambo ambalo linaonyesha heshima kubwa ambayo pande zote mbili zinaweka kwa uhusiano wa pande mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha