

Lugha Nyingine
Spika wa Bunge la China afanya mazungumzo na mwenyekiti wa Bunge la Peru
Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na mwenyekiti wa Bunge la Peru Eduardo Salhuana katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 6, 2025. (Xinhua/Ding Lin)
BEIJING - Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC) amefanya mazungumzo na mwenyekiti wa Bunge la Peru Eduardo Salhuana mjini Beijing siku ya Jumatatu akisema kwamba China inapenda kushirikiana na Peru kutekeleza matokeo muhimu ya yaliyopatikana katika mkutano kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, kusukuma mbele ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Peru, na kunufaisha zaidi nchi hizo mbili na watu wao.
Akibainisha kuwa kuzidisha ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Peru ni matarajio ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili, Zhao amesema vyombo vya kutunga sheria vya nchi hizo mbili vinapaswa kutoa mchango katika kuhimiza maendeleo tulivu na ya muda mrefu ya uhusiano wa pande mbili.
Amesema, Bunge la China linapenda kushirikiana na Bunge la Peru ili kuimarisha mawasiliano kati ya viongozi wa ngazi za juu, kamati maalum, makundi ya urafiki wa pande mbili na wabunge, kuzidisha kufunzana juu ya uzoefu wa utawala wa nchi, kuongeza maelewano na urafiki, na kuungana mkono katika kufuata njia za maendeleo zinazoendana na hali zao halisi za kitaifa.
“Bandari ya Chancay nchini Peru, mradi mkubwa wa ushirikiano kati ya China na Peru, utasaidia kuhimiza ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kati ya China na Peru vilevile China na Latini Amerika,” Zhao amesema, akiongeza kuwa ni matumaini kuwa Bunge la Peru litaendelea kuunga mkono ujenzi wa bandari hiyo.
Kwa upande wake Salhuana amesema Peru inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na inapenda kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati yake na China katika uchumi, biashara, uwekezaji, umeme, miundombinu, utamaduni na sekta nyingine.
“Pande mbalimbali za Bunge la Peru zinaunga mkono kuimarisha uhusiano wa pande mbili na China, na zinapenda kuimarisha mawasiliano ya kirafiki na Bunge la China ili kutoa mchango kwa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili,” Salhuana amesema.
Zhao Leji, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na mwenyekiti wa Bunge la Peru Eduardo Salhuana katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 6, 2025. (Xinhua/Ding Lin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma