

Lugha Nyingine
Msaada wa chakula kuwafikia watu 80,000 nchini Sudan
Msaada wa kibinadamu umeanza kusambazwa jana Jumatatu katika sehemu ya kusini ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum, ukilenga kusaidia watu 80,000 wanaokabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu kutokana na vita vinavyoendelea nchini humo.
Msemaji wa kundi la kujitolea na Chumba Cha Dharura cha Khartoum Kusini, Mohamed Kandasha ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua, kwamba vituo 8 vimeanzishwa ili kutoa msaada kwa maelfu ya wakazi wa maeneo ya Al-Azhari, Al-Ingaz, Ed Hussein na Mayo yaliyoko kusini mwa Khartoum.
Amesema hii ni mara ya kwanza kwa msaada kama huo kutolewa tangu mapigano yalipoanza nchini humo mwezi Mei mwaka 2023, na kwamba msaada huo utatolewa kwa muda wa siku tatu.
Wakati huohuo, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kwa mara ya kwanza limefanikiwa kupeleka msafara wa malori 28 yaliyobeba msaada wa chakula, ikiwemo malori matano yaliyobeba dawa muhimu, katika sehemu hiyo ya kusini ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma