

Lugha Nyingine
China yasema BRICS inayojumuisha nchi nyingi itaonesha umuhimu mkubwa zaidi
(CRI Online) Januari 08, 2025
Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Guo Jiakun amesema, China inakaribisha nchi wanachama wapya kujiunga na BRICS, na kwamba BRICS yenye kujumuisha nchi nyingi itashuhudia umuhimu mkubwa zaidi.
Akizungumza na wanahabari jana Jumanne Bw. Guo amesema Brazil, ambayo ni nchi mwenyekiti wa BRICS wa mwaka 2025, juzi ilitangaza kuwa Indonesia imekuwa nchi mwanachama rasmi wa BRICS, na tarehe 1 mwezi huu, Kazakhstan, Malaysia, Cuba, Bolivia na nchi nyingine nyingi zimekuwa washirika wa BRICS.
Habari zinasema, nchi za BRICS zimeingia kwenye kipindi kipya cha ushirikiano wa BRICS KUBWA, ikionesha umuhimu kubwa katika mshikamano na ushirikiano wa Nchi za Kusini, na uboreshaji wa utawala wa dunia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma