Rais wa Jamhuri ya Kongo akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China

(CRI Online) Januari 08, 2025

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou-Nguesso amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi mjini Brazzaville.

Rais Sassou Nguesso amesema anatarajia msisitizo wa China kwa Afrika utaifanya jumuiya ya kimataifa kuipa kipaumbele zaidi na kuunga mkono Bara la Afrika.

Pia amesema, huu ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing, na ikiwa ni nchi mwenyekiti mwenza, Jamhuri ya Kongo itafanya kila juhudi kutekeleza hatua kumi kuu za ushirikiano na kuhimiza maendeleo zaidi ya ushirikiano kati ya Afrika na China.

Kwa upande wake, Bw. Wang Yi amesema, ziara ya kwanza ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China barani Afrika kila mwanzoni mwa mwaka ni hatua ya kuonyesha kwamba, China inasimama kidete na nchi za Afrika.

Amesema China inapenda kudumisha mawasiliano na uratibu wa karibu na Jamhuri ya Kongo, kutekeleza kikamilifu matokeo ya Mkutano wa FOCAC, kuiunga mkono Afrika kujiendeleza na kuimarisha uchumi wake, na kuiunga mkono Jamhuri ya Kongo kupata maendeleo yake yenyewe na kuongeza ushawishi wake wa kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha