Madaktari wa China waingiza uhai mpya katika huduma za afya Tanzania Zanzibar

(CRI Online) Januari 08, 2025

Kundi la 34 la Timu ya madaktari wa China walioko Tanzania Zanzibar hivi karibuni imetoa mafunzo ya kitaalamu kwa madaktari zaidi ya 30 katika Hospitali ya Wilaya ya Kivunge iliyoko mkoa wa Unguja Kaskazini.

Timu hiyo ambayo ilialikwa na Wizara ya Afya ya Zanzibar, inajumuisha wataalamu kutoka Hospitali ya Umma ya Huai’an No.1 iliyoko mkoa wa Jiangsu nchini China, na wametoa mafunzo ya darasani na kwa vitendo, na kuingiza uhai mpya katika mfumo wa huduma za afya katika eneo hilo.

Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kivunge Dr. Tamim Hamad amewashukuru madaktari hao kwa mchango wao, akisema uwepo wao si tu unatoa huduma bora za afya kwa wagonjwa wenyeji, bali pia unachochea maendeleo ya ujuzi kwa wataalamu wa afya wenyeji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha