Sudan Kusini kuanza tena uzalishaji wa mafuta

(CRI Online) Januari 08, 2025

Sudan Kusini imesema, itaanza tena uzalishaji na usafirishaji wa mafuta ghafi katika soko la kimataifa kupitia Bandari ya Sudan.

Waziri wa Mafuta wa nchi hiyo Puot Kang Chol amesema, serikali imekuwa ikiwasiliana na wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta ikiwemo Wizara ya Mafuta na Nishati ya Sudan, Kampuni ya Mafuta ya Dar (DPOC), ubia wa kampuni za utafiti na uzalishaji wa mafuta, Kampuni ya Mabomba ya Mafuta ya Bashayer, na Shirika la Taifa la Mafuta la China, ili kuhakikisha kuanza tena kwa uzalishaji wa mafuta.

Chol amesema wadau hao wameeleza wasiwasi wao kuhusu utayari wa kiufundi katika kuanza tena uzalishaji huo, ikiwemo nguvu kazi na uhakika wa usalama, masuala ambayo amesema tayari yamefanyiwa kazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha