Huawei yazindua mradi wa uhifadhi wa eneo linalolindwa la baharini nchini Kenya

(CRI Online) Januari 08, 2025

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya China, Huawei, imeshirikiana na Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira ya Asili (IUNC) kulinda eneo la hifadhi lililoko kwenye pwani ya kusini nchini Kenya.

Mradi huo wa miaka mitatu uliozinduliwa Jumatatu wiki hii, unalenga kulinda afya ya ikolojia ya Hifadhi ya Taifa ya Majini ya Kisite-Mpunguti iliyoko Kaunti ya Kwale nchini Kenya.

Mradi huo unaendana na mpango wa Huawei Tech4All na Orodha ya Kijani ya IUNC na lengo lake kuu ni kuboresha usimamizi na ufuatiliaji wa ufanisi wa eneo hilo la majini, ambalo ni makazi ya miamba tumbawe na spishi za kipekee zilizo hatarini kutoweka, wakiwemo kobe wa kijani na pomboo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha