

Lugha Nyingine
CPC chatoa wito wa kujiamini, kustahimili magumu kupambana na ufisadi na kufuata maadili
BEIJING - Chombo cha nidhamu cha Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimetoa wito wa kuongeza imani na uvumilivu kwa hali ngumu katika mapambano ya muda mrefu dhidi ya ufisadi katika hali ya hivi sasa ambayo bado kuna changamoto na utatanishi.
Wito huo umetolewa katika taarifa iliyopitishwa kwenye mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC (CCDI), uliofanyika kuanzia Jumatatu hadi Jumatano wiki hii mjini Beijing.
Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), alihudhuria mkutano huo na kutoa hotuba muhimu.
Mkutano huo umepitia kazi ya ukaguzi wa nidhamu na uendeshaji mashtaka katika mwaka 2024 na kupanga majukumu ya mwaka 2025. Umepitisha ripoti ya kazi iliyotolewa na Li Xi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni katibu wa CCDI, akiwa kwa niaba ya Kamati ya Kudumu ya CCDI.
Wajumbe waliohudhuria mkutano huo wamekubaliana kwamba, chini ya uelekezaji wa hotuba ya Rais Xi, watahimiza kithabiti mapambano dhidi ya ufisadi na kufanya juhudi za kutokomeza vyanzo na mazingira ya ufisadi.
Taarifa ya mkutano umesema, maendeleo makubwa yamepatikana katika kazi ya nidhamu na usimamizi mwaka 2024, ambapo vimefanywa vita vya kupinga desturi za taratibu na urasimu zisizo na maana kwa kulenga hali ya anasa na ubadhirifu
Taarifa hiyo Inasema kuwa kampeni dhidi ya ufisadi iliimarishwa katika maeneo muhimu kama vile mambo ya fedha, nishati na michezo ambapo pia aina mpya za ufisadi na rushwa fiche zilifichuliwa, na watoaji na wapokeaji rushwa waliadhibiwa.
Jumla ya idara 68 zilifanyiwa ukaguzi wa nidhamu wa mara kwa mara mwaka 2024, taarifa hiyo imeeleza.
Taarifa hiyo imetoa wito wa kuimarishwa imani katika kushinda vita vikali dhidi ya ufisadi. Hata hivyo, pia imedhihirisha kuwa hali ya ufisadi "bado ni mbaya na yenye utatanishi."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma