Beijing yafungua kaunta za huduma katika uwanja wa ndege kwa wasafiri wa kigeni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 09, 2025

Kwenye kaunta ya huduma ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, Mfanyakazi akielezea mchakato wa kuiongeza salio kwenye Kitambulisho cha Beijing,  ambacho kina uwezo wa kufanya matumizi mbalimbali,  na kutoa urahisi kwa watalii wa kimataifa  wakati wa kutoa malipo katika usafiri,  kutembelea maeneo ya utalii, na kununua vitu maduniani.   Januari 8, 2025. (Xinhua/Ju Huanzong)

Kwenye kaunta ya huduma ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, mfanyakazi akielezea mchakato wa kuiongeza salio kwenye Kadi ya Beijing (Beijing Pass), ambayo ina uwezo wa kufanya matumizi mbalimbali, na kutoa urahisi kwa watalii wa kimataifa wakati wa kutoa malipo katika usafiri, kutembelea maeneo ya utalii, na kununua vitu madukani Januari 8, 2025. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING – Tokea mwanzo wa mwaka huu, Kaunta za kutoa huduma zote kwenye kituo kimoja zimeanza kufanya kazi kwenye sehemu ya kuwasili kwa wasafiri wa kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing Daxing nchini China.

Kaunta hizo zinatoa huduma za kimsingi zaidi ya 20 katika mambo ya fedha, mawasiliano ya habari, usafiri, utamaduni na utalii, zikihakikisha kwamba wageni watapata urahisi zaidi kwa kufanya utalii na mapumziko, elimu au biashara nchini China. Kwenye kaunta hizo, wasafiri wa kigeni wanaweza kuchukua fedha taslimu kwa kadi zao za benki, kubadilisha fedha na kupata msaada wa kupakua programu za malipo kwa simu za mkononi. Wanaweza pia kununua SIM kadi, kupata huduma ya Wi-Fi ya uwanja wa ndege, kurekebisha ratiba za safari, na kuweka miadi kwenye maeneo ya utalii.

Zaidi ya hayo, wasafiri wanaweza kununua Kadi ya Beijing (Beijing Pass) ambayo ina uwezo wa kufanya matumizi mbalimbali na kutoa urahisi kwa watalii wa kimataifa wakati wa kutoa malipo ya usafiri, kufanya utalii na kununua vitu madukani.

Kaunta hizo pia zinatoa msaada na ushauri wa jinsi ya kununua tiketi za sabwei au kadi za mabasi ya abiria kwenye uwanja wa ndege. Vipeperushi vinavyoonyesha shughuli za kitamaduni, michezo na biashara pia vinaweza kupatikana kwenye kaunta hizo.

Idadi ya jumla ya abiria katika viwanja hivyo viwili vya ndege vya Beijing ilizidi milioni 117 mwaka 2024, ongezeko hili limefikia asilimia 26.2 kuliko mwaka 2023, ambapo abiria wa kimataifa walichukua asilimia 16.8 kati ya idadi hiyo.

China ilitangaza kulegeza kwa kiasi kikubwa sera yake ya kuruhusu wasafiri wa kimataifa wanaopita viwanja vya ndege vya China bila viza Desemba 17, 2024, ikiongeza muda unaoruhusiwa wa kukaa kwa wasafiri wa kigeni wanaofuata matakwa kutoka saa 72 na saa 144 za awali hadi saa 240, au siku 10, ikilenga kuhimiza ufunguaji mlango wa kimataifa na mawasiliano ya kiutamaduni. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha