Lugha Nyingine
China yasema muunganisho wa miundombinu ya mawasiliano unakidhi matarajio ya Nchi za Kusini kwa “Kuwezesha Maendeleo”
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun amesema munganisho wa miundombinu ya mawasiliano ni moja kati ya mambo muhimu ya ushirikiano katika pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lililotolewa na China, na unakidhi matarajio ya Nchi za Kusini kwa "Kuwezesha Maendeleo".
Akijibu swali husika kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatano, Januari 8, Guo amesema katika siku za hivi karibuni, vyombo vya habari vya nchi mbalimbali vimekuwa vikifuatilia matokeo mazuri ambayo China imepata katika ushirikiano wa muunganisho huo, na miradi muhimu kupata maendeleo makubwa.
Guo amesema China imekuwa msukumo muhimu wa kuunganishwa kwa dunia, akiongeza kuwa, China itaendelea kushikilia kanuni ya kujadiliana, kujenga kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja, na kupanua zaidi maeneo ya maendeleo ya kunufaishana yenye kiwango cha juu, himilivu na endelevu zaidi.
Aidha, amesema China imekuwa ikichangia maendeleo ya Dunia kupitia kunufaika kwa pamoja kutokana na maendeleo bora ya hali ya juu na ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, ikichangia mambo ya kisasa na Nchi za Kusini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma