Idadi ya vifurushi vilivyosambazwa nchini China mwaka 2024 yazidi bilioni 170

(CRI Online) Januari 09, 2025

Mkurugenzi wa Shirika la Posta nchini China Bw. Zhao Chongjiu jana Jumatano kwenye mkutano wa kazi wa Shirika hilo amesema, mwaka 2024 idadi ya vifurushi vilivyosambazwa nchini humo ilifikia bilioni 174.5, ikiwa ni ongezeko la asilimia 21 kuliko mwaka 2023.

Amesema mapato yaliyopatikana kutokana na biashara ya usambazaji wa vifurushi yalifikia Yuan trilioni 1.4, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13 kuliko mwaka jana.

Bw. Zhao amesema, inakadiriwa kuwa mwaka 2025, idadi ya vifurushi vitakavyosambazwa itafikia bilioni 190, na mapato yatafikia yuan trilioni 1.5.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha