Lugha Nyingine
UN: Juhudi za kibinadamu katika Ukanda wa Gaza ziko ukingoni kuporomoka
(Picha/CRI)
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) anayeshughulikia mambo ya kibinadamu ambaye pia ni mratibu wa misaada ya dharura Tom Fletcher ametoa taarifa Januari 6 akionya kuwa juhudi za Umoja wa Mataifa za kutoa misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza ziko ukingoni kuporomoka.
Amesema katika siku kadhaa zilizopita, mashambulizi mengi dhidi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yametokea katika ukanda huo, na kwamba sasa hakuna utaratibu wa kawaida wa kijamii katika eneo hilo.
Aidha, amesema kuwa wafanyakazi hao wa utoaji misaada wamekashfiwa na taarifa za serikali ya Israel, hata kumekuwa na dhana yenye kushtua kwamba kulinda misafara ya magari ya misaada ni hatari lakini kuishambulia ni salama.
Ametoa wito kwa nchi wanachama wa umoja huo kushikilia msimamo wa kulinda usalama wa raia na operesheni za kibinadamu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma