Lugha Nyingine
Rais wa Chad akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China kuendeleza ushirikiano wa pande mbili
Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), kwenye mkutano wao mjini N'Djamena, Chad, Januari 8 , 2025. (Xinhua/Han Xu)
N'DJAMENA - Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi mjini N'Djamena jana Jumatano kujadili kuendeleza ushirikiano wa pande mbili ambapo Mahamat amemuomba Wang kuwasilisha salamu zake za dhati na heshima kwa Rais Xi Jinping wa China.
“Rais Xi ni kiongozi mwenye upeo wa mbali, anayeongoza China kuelekea mafanikio ya ajabu ya kiuchumi na kufanya kazi muhimu kwenye jukwaa la kimataifa,” Mahamat amesema.
Ameipongeza China kuandaa kwa mafanikio Mkutano wa Kilele wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing mwaka jana, ambao amesema umeendeleza kwa kiasi kikubwa uhusiano kati ya China na Afrika.
“Ushirikiano wa China na Afrika siku zote unafuata kanuni za kimsingi za kuheshimiana, kuwa na usawa, na kunufaishana, ukileta matokeo yenye matunda,” amesema. Pia ameeleza shukrani zake kwa China kwa uungaji mkono wake wa kudumu kwa maendeleo ya Afrika, hususan maendeleo ya Chad.
“China ni mshirika muhimu wa kimkakati wa Chad na rafiki wa kutegemewa, uhusiano wao wa pande mbili ni mfano wa kuigwa katika kuheshimiana na kufanya ushirikiano wa kunufaishana,” Mahamat amesema.
Amesisitiza kuwa, Chad inaunga mkono kithabiti juhudi za China za kulinda ukamilifu wa ardhi yake na kufikia muungano wa taifa, na kupinga uingiliaji katika mambo yake ya ndani.
Kwa upande wake, Wang amewasilisha salamu za uchangamfu za Rais Xi kwa Rais Mahamat.
Amesema kuwa baada ya rais Mahamat kuingia madarakani, ziara yake ya kwanza nje ya nchi yake ilikuwa ni China na kuhudhuria mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing, huku ziara hiyo ilifanikiwa kufanyika na kuchangia mafanikio ya mkutano huo.
Wang amesema kwenye ziara hiyo nchini China, wakuu wa nchi hizo mbili kwa pamoja waliinua uhusiano wa pande mbili kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati, ukiingia katika kipindi kipya cha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma