Majibizano ya risasi yasikika katika mji mkuu wa Chad

(CRI Online) Januari 09, 2025

Majibizano ya risasi yamesikika katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena, jana jioni.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, majibizano hayo ya risasi yametokea kati ya wanajeshi wa serikali ya Chad na wapiganaji wa kundi la Boko Haram, na sasa hali imetulia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Abderaman Koulamallah amesema hali ya usalama kwa sasa imedhibitiwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha