

Lugha Nyingine
Mtaalamu wa Zimbabwe asema ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China barani Afrika inaonyesha uhusiano imara wa China na Afrika
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti na Uhifadhi wa Nyaraka cha Kusini mwa Afrika, Munetsi Madakufamba amesema, ziara inayoendelea ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China barani Afrika ni ishara ya uhusiano imara kati ya China na Afrika.
Akizungumza na Shirika la Habari la China, Xinhua, Mudakufamba amesema kwa miaka 35 mfululizo, mawaziri wa mambo ya nje wa China wamelichagua Bara la Afrika kuwa kituo cha kwanza cha ziara zao nje ya nchi kila mwanzoni mwa mwaka, ikionyesha sera isiyobadilika ya China na kuitambua Afrika kama mshirika muhimu.
Amesema hivi karibuni China imetekeleza sera ya kutotoza ushuru kwa nchi 33 zilizo na uchumi mdogo barani Afrika kwa bidhaa zao, na kuboresha biashara na Afrika na pia kuongeza fursa kwa wafanyabiashara wa Afrika.
Amesema ziara hiyo inayoendelea ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China katika nchi za Namibia, Jamhuri ya Kongo, Chad na Nigeria inadhihirisha nia ya China ya kuimarisha kwa kina urafiki wa jadi na nchi za Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma