Lugha Nyingine
Xi Jinping aongoza mkutano wa viongozi wa CPC wa kuokoa maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea Xizang
BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameongoza mkutano wa viongozi wa CPC uliofanyika jana Alhamisi ili kufahamishwa hali halisi na kupanga utoaji wa msaada wa kuokoa maafa ya tetemeko la ardhi la ukubwa wa 6.8 lililotokea katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang mapema wiki hii.
Mkutano huo wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya CPC umesisitiza kuwa kazi ya kuokoa maafa iko katika kipindi muhimu na lazima kufanya kazi hiyo bila kulegalega.
Mkutano huo umesisitiza kuwa, juhudi lazima zifanywe ili kuhakikisha ushindi wa mwisho unapatikana katika vita hivyo vigumu dhidi ya maafa.
Mkutano huo umefanya majumuisho ya kazi za kuokoa maafa zilizofanyika hadi sasa, ukieleza kuwa maeneo na idara husika zimeitikia kwa haraka na kwa ufanisi, zikishindana na wakati kuokoa maisha na kupunguza vifo na majeruhi.
Mkutano huo umesisitiza haja ya juhudi zote kutibu majeruhi, kukidhi mahitaji ya kimsingi ya maisha ya wale walioathiriwa na tetemeko hilo la ardhi, na kuhakikisha wanaweza kujisitiri kwenye joto katika siku zote za majira ya baridi.
Mkutano huo umetoa wito wa kuharakishwa kwa ukarabati wa miundombinu na kusafisha vifusi ili kurejesha mazingira ya kawaida ya kazi na maisha katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko hilo haraka iwezekanavyo.
Pia umesisitiza umuhimu wa kutoa habari na taarifa zenye mamlaka, kuimarisha uhimilivu wa tetemeko la ardhi wa nyumba na miundombinu katika maeneo muhimu, na kuongeza uwezo wa kuitikia kazi ya kuokoa maafa.
Mkutano huo umewataka maofisa wa ngazi zote washikilie kazi zao kwenye mstari wa mbele na kufanya juhudi zozote katika kutekeleza majukumu yao na wajibu wao, mkutano huo umeongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma