Maendeleo ya kijani "kielelezo kingine cha ushirikiano kati ya China na Afrika"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 10, 2025

BEIJING – Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Guo Jiakun amesema kuwa, China na Afrika ni washirika wanaofanya vitendo halisi katika kukabiliana na tabianchi na kutafuta maendeleo ya kijani, amedhihirisha kuwa maendeleo ya kijani yatakuwa kielelezo kingine cha ushirikiano kati ya China na Afrika.

Msemaji huyo amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Alhamisi wakati alipotoa maoni yake kuhusu ripoti za vyombo vya habari vya Afrika, akisema kwamba kuimarika kwa uhusiano kati ya China na Afrika na ahadi za kunufaika pamoja na mafanikio ya ujenzi wa mambo ya kisasa kumeweka msingi imara kwa ajili ya kuelekea mabadiliko ya kijani barani Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye yuko ziarani Afrika, amesisitiza kuwa China inaunga mkono maendeleo ya kijani barani Afrika na itajikita katika kushirikiana na Afrika kwa kuhimiza ujenzi wa mambo ya sasa unaotilia maanani kulinda mazingira ya asili, ameeleza Guo.

“Kwa kupitia kuiga uzoefu wa China katika miradi ya kulinda Misitu ya Mikoa ya Kaskazini mwa China, nchi za Afrika zimetoa pendekezo la “Ukuta Mkuu wa Kijani” ili kuzuia jangwa la Sahara lisienee tena”, Guo amesema.

Ameongeza kuwa China imetekeleza mamia ya miradi katika sekta ya nishati safi barani Afrika. Uwezo wa mashine zilizofungwa kwenye vituo vya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya jua zilizojengwa kwa pamoja na China na Afrika umefikia gigawati jumla ya 1.5.

Amesema, ushirikiano katika teknolojia ya kijani, kama vile nishati ya upepo, nishati ya jotoardhi na nishati ya jua, umetoa nguvu kubwa katika mpito wa kuelekea nishati mbadala wa nchi za Afrika.

Ameeleza kuwa, miradi 30 ya nishati safi itazinduliwa barani Afrika, maabara 30 za pamoja zitaanzishwa, na pande hizo mbili zitashirikiana katika satalaiti za kuhisi kwa mbali na utafiti kwenye Sayari ya Mwezi na anga ya juu ya kina.

"Maendeleo ya kijani yatakuwa kielelezo kingine cha ushirikiano kati ya China na Afrika," amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha